Comments


Mary J Blige ampa talaka mume wake

Mwanamuziki mashuhuri wa miondoko ya PoP na Soul, Mary J. Blige, amempatia rasmi aliyekuwa mume wake Martin Kendu Isaacs Talaka ya kuvunja rasmi ndoa yao kutoka mahakamani na kuweka wazi kupitia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Blige (45) alieleza kuwa amekuwa akiteseka mara nyingi katika ndoa yake kutokana na vitendo alivyokuwa akivifanya Kendu na kwa sasa ameshindwa kuvumilia na kuhamua kufanya maalum kwa kuipeleka kesi hiyo katika mahakama zinazoshughulikia maswala ya ndoa.

Mwanamama huyo aliyewahi kutamba na kibao ‘Be Without You’ cha aliwaambia waandishi wa habari kuwa mara nyingi wamekuwa wakigombana lakini wanafamilia waliingilia kati na kuyamaliza na kwa sasa hafikirii tena kutengua uamuzi wake.

“Nadhani kwa sasa hakuna atakayetengua uamuzi niliochukua kwa kuwa mara zote familia imekuwa ikimtetea kendu, na tumejitahidi lakini naona matumaini ya kurekebishika yamepotea kabisa”, alisema Blige

Blige pamoja na Isaacs ambaye pia ni meneja wake walifunga ndoa mwaka 2003 na aliweka wazi kuwa na matatizo ya kifamilia rasmi mwaka 2014 na kueleza jinsi Kendu akimpiga mara kwa mara na kuongeza kuwa alikuwa akishindwa kuchukua maamuzi ukiachana na mambo ya muziki lakini pia ni mume wake.

Mwaka 2012 Blige alihojiwa katika kipindi cha The Wendy Williams Show, na alisema kuwa “kila kitu kipo sawa kabisa, sina tatizo lolote na mume wangu, nayafurahia maisha ya ndoa na huwa hatupendi kujiweka mbele za watu sana lakini kila mmoja wetu ana mapenzi ya kweli ndani yake.

Mwaka mmoja baadae alihojiwa na Telegraph na kueleza kuwa “kila mmoja wetu ana maarafiki zake na Isaacks ndio amegawa makundi haya ‘wanawake wote marafiki zangu na wanaume wote rafiki zake’ na imekuwa ikinigusa sana katika maisha yangu ya ndoa.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system