Comments


Paul Scholes amkosoa Louis van Gaal kwa mara nyinginekuhusu mfumo wa United,

 

Klabu ya Manchester United ya Uingereza Usiku wa October 28 ilitolewa rasmi katika michuano ya Kombe la Capital One na Middlesbrough kwa mikwaju ya penati 3-1 baada ya kucheza kwa dakika 120 na kutoka sare ya kutofungana. October 29 kiungo wa zamani wa klabu hiyo Paul Scholes ameeleza ya moyoni kuhusu kocha Louis van Gaal na mwenendo wa timu.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri kocha wa Man United Louis van Gaal anatajwa kutokuwa na mahusiano mazuri na wachezaji yaani sio rafiki na wachezaji yeye pamoja na mbinu zake za ufundishaji, Paul Scholes ambaye aliwahi kucheza Man United kwa muda mrefu ametoa ya moyoni kuwa asingefurahia kucheza katika timu hiyo chini ya Van Gaal.
465222378-377913
“Timu ina kosa ubunifu, ni timu ambayo huwezi penda kucheza nayo inaonekana kama Van Gaal hataki timu yake ishinde na inaonekana kama sio timu kiukweli nisingefurahia kucheza timu hiyo”>>> Paul Scholes
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system