Comments


TASWA YA PIGWA 2-1 NA NSSF


TIMU ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC imeshindwa kutamba mbele ya wenzao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) baada ya kulala kwa mabao 2-1 katika mchezo maalumu wa kuadhimisha miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Katika mchezo huo uliofanyika jana Uwanja wa Bora, Kijitonyama katika Manispaa ya Kinondoni, mabao ya NSSF yalifungwa na Linus Bwegoge na Mzee Mwinyi wakati la Taswa lilifungwa na Khatim Naheka kwa njia ya penalti. Kama si Saidi Seif kukosa penalti, Taswa FC ingeweza kusawazisha bao.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki wa kati wa NSSF, Khalfan Waziri kumwangusha Zahoro Mlanzi aliyecheza vizuri akishirikiana na Angetile Osiah.
Mbali ya Osiah, Seif, Julius Kihampa na Mohammed Akida nao walikosa nafasi nyingi za kufunga katika mchezo huo ambao wachezaji, Wilbert Molandi, Nurdin Mponda, Jabir Johnson na Simon Sonda walicheza vizuri.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema hawajaridhika na kipigo hicho cha mara ya kwanza tangu kuanza kwa mwaka huu na kujipanga upya kwa ajili ya mchezo wa marudiano
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system