Comments


HATUA STAHIKI KUKOMESHA MAUAJI



MWAKILISHI wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), Balozi Tuvako Manongi amesema, hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), tofauti na inavyofikiriwa na baadhi ya watu.
Balozi Manongi aliyekiri kuwa mauaji hayo yamekuwa janga la taifa alisema serikali imekuwa ikichukua hatua dhidi ya wauaji ikiwemo kuwafikisha mahakamani ambapo, watu kadhaa waliothibitika kuhusika na mauaji hayo walifungwa huku wengine wakiendelea kushikiliwa na Polisi kwa uchunguzi.
Akizugumza na wanahabari jijini New York, Marekani, Balozi Manongi aligusia filamu iitwayo The Boy from Geita (Mvulana kutoka Geita) iliyotazamiwa kuoneshwa kwenye makao makuu ya UN jana, akisema filamu hiyo ina maudhui yanayoonesha kuwa serikali haijachukua hatua zozote za kupiga vita mauaji hayo, jambo ambali si kweli.
“Filamu hiyo haikuzingatia juhudi zinazochukuliwa na serikali, wananchi, wanasiasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia na wanaharakati wengine kupambana na mauaji hayo,” Balozi Manongi alisema. 
Aidha, alisema Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiyakemea huku serikali yake ikihakikisha yanadhibitiwa kwa mafanikio makubwa.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system