Comments


NEC: Raia Wa Kigeni Zaidi Ya Elfu 3 Waliandikishwa




Mwananchi akijiandikisha kupata kitambulisho cha kupigia kura.
Mwananchi akijiandikisha kupata kitambulisho cha kupigia kura.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ilibani kuwa jumla ya watu 3,870 walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo vitambulisho vyao vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya daftari la kudumu la kupiga kura.
Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani, amebainisha hayo wakati akizungumza katika mkutano wa kushauriana na viongozi wa vyama vya siasa uliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Bw. Ramadhani amesema katika kuelekea uchaguzi, Tume imeandaa vituo vya kupigia kura 65,105, ambapo Tanzania Bara ina vituo 63,525 na Zanzibar vituo 1,580, ambapo kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wapiga kura 450.
Amesema kituo kitakacho kuwa na wapiga kura zaidi ya 500 kitagawanywa katika vituo viwili.
Mpaka sasa tume imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa ambavyo havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu, karatasi za matokeo na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake, ila vinatarajiwa kusambazwa hivi karibuni.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system