Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Kikwete, leo amezindua rasmi Mtambo wa Kufua Umeme wa Gesi Asilia wa Kinyerezi (Namba Moja).
Mtambo huo uliojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 400 na kampuni kutoka Norwey, unauwezo wa kuzalisha Megawati 150.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Kikwete amesema serikali ilikuwa imeweka kipaumbele katika suala la upatikanaji umeme wa uhakika, kwa kuwa bila nishati hiyo hakuna Maendeleo ya kiuchumi.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq, akizungumzia kuanza kazi kwa mtambo huo, amewaomba wananchi kuwa walinzi wa miundo mbinu ya umeme wa gesi asilia kwa kuwa inapita katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment