Comments


Obama aongeza muda wa majeshi ya marekani kuwepo nchini Afghanistan



Image copyrightGetty
Image captionObama amesema kuwa majeshi ya Afghanistan haviwezi kuhimili vitisho vya Taliban
Rais wa Marekani,Barack Obama ametangaza kuongeza muda wa majeshi ya Marekani kuwepo nchini Afghanistan.
Amesema kuwaTakriban wanajeshi 10,000 wataendelea kubaki nchini humo kwa kipindi hasa cha mwaka ujao.
Obama amesema vikosi vya Afghanistan havina nguvu bado ya kupambana na tishio linaloongezeka kutoka kwa wanamgambo wa Taliban.
Hatahivyo Washington pia imesema inatarajia kuendelea kuungwa mkono na washirika wake, kwa kuwa mazungumzo kuhusu suala hili yamekwisha anza.
Wakati ambapo Rais Obama anaondoka madarakani mwaka 2017, kutakuwa bado kuna wanajeshi 5000 nchini Afghanistan.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system