Comments


kuelekea mchezo wa kesho Mbeya city vs Simba hapatoshi

Boban & Kaseja 
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Haruna Moshi ‘Boban’ atacheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara akiwa na Mbeya City siku ya Jumamosi hii katika uwanja wa Sokoine, Mbeya wakati wenyeji timu ya Mbeya City FC itakapowavaa Simba SC. 
Boban ambaye amewahi kushinda mataji manne ya ligi kuu akiwa na Simba miaka ya 2003, 2004, 2007 na 2009/10 alikuwa nje ya kikosi cha City tangu  aliposainiwa mwaka huu kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kusaka nafasi ya kucheza mpira wa kulipwa. 
Tayari ameungana na wachezaji wenzake katika kikosi cha City ambacho kimeanza vibaya msimu huu. Mbeya City imeshinda mara moja, imepoteza michezo minne na kuambulia sare katika gemu moja, itacheza na Simba kwa mara ya kwanza msimu huu ikiwa na ‘washindi’, Juma Kaseja, mlinzi wa kulia Haruna Shamte ambao pia wamewahi kushinda ubingwa wa ligi kuu wakiwa Simba katika miaka tofauti. 
Image result for simba vs mbeya cityImage result for simba vs mbeya cityWachezaji hao watatu waliachwa ‘kimizengwe’ mara baada ya Simba kumaliza katika nafasi ya tatu ya ligi kuu bara msimu wa 2012/13. Haruna aligombana na aliyekuwa mkufunzi mkuu wa Simba, Mfaransa, Patrick Liewig (sasa ni kocha wa Stand United), Kaseja hakuwa tayari kusaini kwa malipo ‘kiduchu’, wakati Shamte hakupewa mkataba 
Mechi ya kwanza ya Haruna katika ligi kuu bara Jumamosi hii itanogesha pambano la ‘kukata na shoka’ katika uwanja wa Sokoine, Mbeya. Nitapenda pia kuona vita ya Shamte ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambao hucheza kwa nguvu huku wakishambulia na kukaba mawings wa timu pinzani. Kaseja, Shamte, Boban vs Simba hii ni mechi ngumu kwa Simba SC. Hakika watataka kulipa kisasi kwa sababu……..

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system