Comments


Baada ya kuzirai Hatimae apata fahamu tena.



Image copyrightAP
Image captionOdom akiichezea La Clippers
Mchezaji wa zamani wa mpira wa vikapu katika ligi ya NBA nchini Marekani Lamar Odom hatimaye amepata fahamu siku tatu baada kuzirai ndani ya danguro katika jimbo la Nevada.
Msemaji amesema kuwa bwana Odom alizungumza na kutoa maamkuzi ya kidole katika kitanda chake cha hospitalini.
Alikuwa katika mashine ya usaidizi baada ya kupatikana siku ya jumanne akitokwa na damu puani na mdomoni.
Image copyrightReuters

Image captionOdom na aliyekuwa mkewe Khloe Kardashian
Wafanyikazi wa danguro la Love Ranch,huko Crystal,Nevada wamesema kuwa bwana Odom alikuwa katika danguro hilo kwa siku kadhaa na amekuwa akila dawa za kulevya aina ya cocaine pamoja na zile za kuongeza hamu ya ngono.
Odom aliwahi kushinda taji la ubingwa akiichezea Los Angeles Lakers.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system