Comments


Mita 200 hairuhusiwi kufanya mkutano


Mahakama: >>Mita 200 hairuhusiwi kufanya mkutano

Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,  imeamua kuwa watu hawapaswi kufanya mkutano katika eneo la umbali za mita 200 kutoka kituo cha kupiga kura, kama inavyoelezwa katika kifungu cha 104 cha Sheria ya Uchaguzi.
 
Uamuzi huo ulitolewa jana na jopo la majaji watatu kufuatia kesi ya kikatiba iliyowasilishwa na mgombea ubunge wa viti maalum katika jimbo la Kilombero (Chadema), Amy Kibatala.
 
Kupitia hati ya kiapo cha dharula, Oktoba 16, mwaka huu Amy akitaka mahakama hiyo itoe tamko kuhusu maana halisi na kusudio la sheria namba 104 kifungu kidogo cha (1) sura ya 343.
 
Jopo la majaji Sakieti Kihiyo (Mwenyekiti), Lugano Mwandambo na Aloysius Mjujulizi iliamuru kuwa ni marufuku kufanya mkutano mita 200 au baada ya umbali huo kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.
 
Uamuzi huo utagusa maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar.
 
Majaji hao walitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza maombi ya kuhusu tafsiri ya kifungu cha 104 cha Sheria ya Uchaguzi, kukaa kwa utulivu mita 200 kutoka vituo vya kupigia kura wakati tukio hilo linaendelea.
 
Shauri hilo lilifunguliwa mahakamani hapo dhidi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi (Nec).
 
Akisoma uamuzi kwa niaba ya jopo hilo, Jaji Kihiyo alisema baada ya kupitia hoja za mlalamikaji na upande wa walalamikiwa, mahakama imeona kwamba mgombea huyo (Amy) hajafanikiwa ombi la kuruhusiwa kukaa mita 200. 
 
Kwa ujumla mlalamikaji hakufanikiwa maombi yake, tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) kwa kuwa ni katazo, hakuna mtu anayeruhusiwa kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura suala la kwamba watakaa kwa utulivu hilo halipo alisema Jaji Kihiyo wakati akifafanua uamuzi wa jopo hilo.
 
Alisema hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kukaa mita 200 na hata zaidi ya umbali huo wakati tukio la upigaji kura na kuhesabu likiendelea.
 
Akizungumzia uamuzi huo, wakili Peter Kibatala, aliyemwakilisha Amy, alisema hakuridhika na uamuzi huo na kwamba kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu haitakuwa na faida, lakini atakata rufaa Jumatatu ijayo kwa ajili ya chaguzi za miaka ijayo ili iwekwe kwenye kumbukumbu ya mahakam
©©®

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system