Comments


Makanisa Yaanza Kufuta Ibada Siku Ya Uchaguzi Mkuu

Askofu Severin Niwemugizi.
Askofu Severin Niwemugizi.
Baadhi  ya Makanisa nchini Tanzania yameanza kufuta ibada inayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 ili wananchi wapate fulsa ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa  uhuru na amani. Hatua hiyo inafuatia wakati zikiwa zimesalia siku kadhaa  kufanyika uchaguzi mkuu
Aidha,baadhi ya makanisa nchini Tanzania yametoa ruhusa maalum kwa viongozi wa kanisa kuendesha ibada zao Jumamosi tarehe 24 ya mwezi huu wa Oktoba 24 2015 badala ya Jumapili tarehe 25 ili kutoa nafasi kwa waumini wao kushiriki shughuli kubwa ya upigaji kura.
Makamu wa rais wa Baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amesema kuwa ibada haipaswi kuzuia haki ya kimsingi na kikatiba ya waumini .
“Si utaratibu wa kawaida kwa sababu kama baraza hatujakaa, lakini kila askofu anawajibika ndani ya jimbo lake, hivyo anaweza kutoa fursa hiyo.

Katika  hatua  nyingine Rais Jakaya Mrisho Kikwete anayeelekea kukamilisha muhula wake wa pili atatoa nafasi kwa rais wa tano kuchukua madaraka mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.“Hata mimi katika jimbo langu la Rulenge Ngara, nimetoa kibali hicho kwa makanisa yote” amenukuliwa akisema Askofu Severini.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system