Comments


Stars wahitaji bilioni2 kuivaa Algeria

Taifa Stars
Safari ya Taifa Stars kuvuka kizingiti cha awali kwenda kucheza fainali za Kombe la Dunia, itaigharimu shilingi bilioni 2 kwa mechi mbili-ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria baadaye mwezi ujao, imefahamika.
 
Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde iliyopewa jukumu la kufanya maandalizi ya mechi hizo, mbili ilisema fedha hizo zitachangwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini.
 
Katibu wa kamati hiyo, Teddy Mapunda akitoa mchanganuo mfupi wa matumizi ya fedha hizo jana mbele ya waandishi wa habari, alisema zitatumika kwa ajili ya kambi ya timu hiyo ndani na nje ya nchi.
 
Kadhalika, kamati imeona kuna ulazima wa kukodi ndege maalumu kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Novemba 17 mwaka huu, mjini Algiers.
 
"Malengo yetu ni kukusanya Shilingi bilioni 2. Tutafungua akaunti maalumu ili kila kiasi cha fedha kitakachoingia kionekana kilikotoka," alisema Mapunda.
 
Alisema fedha hizo pia zitatumika kwa ajili ya maandalizi mengine muhimu ya timu ili iweze kufanya vizuri kwenye mechi hizo.
 
Stars imevuta hatua moja ya awali baada ya kuitoa Malawi kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda nyumbani 2-0 na kupoteza ugenini 1-0.
 
Kuhusu kambi ya timu hiyo, Mapunda alisema baadhi ya wajumbe watasafiri kwenda Oman, Dubai na Afrika Kusini kwa ajili ya kuangalia sehemu nzuri ya kuweka kambi.
 
"Bado hatujaamua kambi itakuwa wapi, tunachofanya kwa sasa ni kutafuta sehemu.
 
"Watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi 100, ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji na masoko na maboresho ya kambi," aliongeza.
 
Naye Mratibu wa Taifa Stars, Msafiri Mgoyi alisema uteuzi wa kambi ya timu hutokana na mjumuisho wa mambo mengi na siyo hali ya hewa tu.
 
Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kupeleka mbele baadhi ya mechi za ligi kuu Bara ili kupisha kambi ya siku 12 itayoanza Novemba Mos

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system