Comments


WAMENIFUNGULIA NJIA YA KWENDA ULAYA>SAMATTA




Mbwana Samata.
Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Samatta, amesema kwambKa kuteuliwa kwake kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka kumemfungulia njia ya kwenda kukipiga Ulaya.
 
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilitangaza orodha ya majina ya wachezaji watakaowania tuzo hiyo na Samatta ndiye pekee Afrika Mashariki.
 
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka Lubumbashi, Kongo jana, Samatta alisema kwamba mbali na kumsafishia njia yeye binafsi, anaamini uteuzi huo pia umesaidia kutangaza jina la Tanzania kimataifa.
 
Alisema hatua hiyo aliyofikia imetokana na juhudi za kujituma anapokuwa katika klabu yake na kwenye kikosi cha Stars.
 
"Najisikia furaha, kwani uteuzi huu pia umesaidia kuitangaza Tanzania kimataifa," alisema Samatta aliyewahi kucheza Simba na African Lyon kabla ya kutimkia Kongo DRC.
 
Hata hivyo pamoja na mafanikio aliyopata akiwa na TP Mazembe, amebainisha wazi kuwa hatakuwa tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo mara ule wa sasa utakapomalizika.
 
"Kwa sasa nahitaji kutimiza ndoto zangu, ningependa kucheza Ulaya," alisisitiza Samatta ambaye mkataba wake na TP Mazembe unatarajiwa kumalizika mwezi Aprili mwakani.
 
Alisema pia kwa muda wa miaka minne ambayo ameichezea TP Mazembe amepata uzoefu wa kucheza mechi mbalimbali za kimataifa na kujenga kipaji chake, huku pia akijifunza mambo mengi ya maisha. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system