Comments


Martial angara tuzo ya mchezaji bora wa mwezi

Klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa
miaka miwili sasa ilikuwa haijawahi kutwaa tuzo ya
mchezaji bora wa mwezi. Tuzo ya mchezaji bora
wa mwezi kwa sasa imechukuliwa na Anthony
Martial mshambuliaji mwenye umri mdogo ambaye
aliweka rekodi ya kuuzwa kwa gharama ya juu
katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August.
Anthony Martial anakuwa mshambuliaji wa kwanza
wa Man United kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora
wa mwezi kwani mara ya mwisho mchezaji wa
Man United kutwaa tuzo hiyo kabla ya Anthony
Martial alikuwa ni Robin van Persie ambaye alitwaa
tuzo hiyo mwezi April 2013.
Mshambuliaji huyo kinda wa kifaransa alijiunga na
Man Unite d katika dirisha la usajili la majira ya joto
2015 akitokea AS Monaco ya Ufaransa kwa dau la
uhamisho wa pound milioni 36, hivyo October 16
ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji wa
kwanza wa Man United kutwaa tuzo hiyo katika
kipindi cha miaka miwili. Kwa upande mwingine wa shilingi kocha wa

Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino
ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system