Comments


INGS, GOMEZ NJE MSIMU



Image result for klopp liverpoolDanny Ings ruled out for the season as Liverpool manager Jurgen Klopp suffers second injury blow


MENEJA mpya wa Liverpool Jurgen Klopp anaanza himaya yake kwa kuvamiwa na Jinamizi zito baada ya Wachezaji wake Wawili kutupwa nje ya Msimu baada kuumia vibaya.
Ripoti kutoka katika klabu hiyo imethibitishwa kuwa Straika wao waliemnunua mwanzoni mwa Msimu huu kutoka Burnley, Danny Ings, ameumia vibaya Goti lake kwenye Mazoezi Klabuni Liverpool Jana Jumatano.
Ings aliichezea England kwa mara ya kwanza Jumatatu Usiku Ugenini walipoifunga Lithuania 3-0.
Ings sasa anaungana na Chipukizi Joe Gomez ambae nae pia aliumia Goti hivi Juzi na kutambulika kuwa ataukosa Msimu mzima.
Jumamosi Liverpool wanasafiri kwenda London kucheza na Tottenham katika Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Meneja Klopp ambae sasa amebakiwa na Mastraika Wawili tu ambao wako fiti na hao ni Divock Origi na Daniel Sturridge.
Majeruhi wengine wa Liverpool ni Nahodha wao Jordan Henderson ambae amevinjika mfupa wa Kidole cha Mguu pamoja Christian Benteke na Roberto Firmino.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system