Comments


Nape apata ajali

Zimeenea picha pamoja na taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu gari ya Kada wa CCM, Katibu wa Itikadi na Uenezi, na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama Mkoa wa Lindi, Nape Moses Nnauye kupata ajali…
simu yake imepokelewa na Dereva wake, na hiki ndicho alichokieleza juu ya ajali hio iliyomkumba Nape Nnauye.
.

“Ni kweli amepata ajali alfajiri ya leo lakini hajambo, alikuwa anaendesha mwenyewe gari… amepata ajali maeneo ya SOMANGA, barabara kuu ya kutoka Dar kwenda Lindi, ilikuwa saa 12 alfajiri..” >>> Dereva wa Nape Nnauye.

“Tulitoka Dar es Salaam saa kumi na robo tunakwenda Jimboni Lindi, alikuwa kwenye gari pekeyake mimi nilikuwa nyuma yake.. ana jeraha dogo, mkanda umemchubua mkono wa kulia kidogo… Tumetoka Hospitali, hana tatizo lolote na yuko kwenye Kikao kwa sasa“

Kuhusu hali ya gari je? >>> “Gari imeharibika sana, ni toyota Land Cruiser na iko kwenye Kituo cha Polisi Somanga“

Alihitimisha kwa kusema hivyo dereva wa Nape , hivyo basi taarifa zaid utazid kuzipata katika vyombo mbalimbali  vya habari

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system