Shirikisho la kandada nchini Ujerumani limekana vikali madai kuwa lilitumia rushwa ili kupata nafasi ya kuandaa kombe la dunia la mwaka 2006.

Katika taarifa yake shirikisho hilo lilisema kuwa shutuma zilizotolewa na gazeti la Der Spiegel hazikuwa na msingi wowote.

Gazeti hilo ambalo halikusema lilitoa wapi habari hizo lilisema kuwa karibu dola milioni sita zilitumika kununua kura kutoka kwa baadhi ya wanachama wa kamati kuu ya FIFA ili Ujerum
ani ipewe nafasi ya kuandaa kombe hilo.
FIFA inasema kuwa madai hayo dhidi ya Ujerumani yanatiliwa maanani na yatakuwa sehemu ya uchunguzi wa ufisadi katika mchezo wa kandanda duniani
0 comments:
Post a Comment