Comments


SIMBA TUNA POINT TATU JUMAMOSI ZIDI YA MBEYA CITY


14th October 2015
Chapa
Kocha wa Simba, Dylan Kerr.
Simba haikuwahi kupata ushindi kwenye mechi za ligi kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kwa miaka mitatu, lakini msimu huu wakati ligi ikiwa bado mbichi, tayari imeshavuna pointi sita na kuvunja mwiko wa kutopata ushindi kwenye uwanja huo.
 
Lakini pia kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa misimu miwili mfululizo, Simba haijawahi kuibuka na ushindi na Jumamosi hii inarudi tena kwenye uwanja huo kujaribu kuvunja mwiko kama ilivyofanya Mkwakwani.
 
Kocha wa timu hiyo Dylan Kerr, anafahamu mazingira magumu ya kucheza kwenye Uwanja wa Sokoine, lakini hilo halionekani kuwa tatizo kwake, kwani dhamira yake ya kuvunja mwiko wa ushindi iko palepale.
 
Simba, mabingwa mara 18 wa Bara, watakuwa na mtihani mgumu kama wageni wa timu isiyotabirika ya Mbeya City.
Kerr amesema siyo tu wamepania kuvunja mwiko huo, lakini dhamira yao ni kushinda kila mchezo wa ligi. 
 
"Tayari tumevunja mwiko Tanga, sasa tunasubiri muda ufike tuvunje mwiko mwingine Mbeya," alitamba Manara.
 
Kerr alisema wako Mbeya kuvuna pointi sita katika michezo miwili dhidi ya City na Prisons.
 
"Tumekuja kusaka pointi sita hapa (Mbeya), tutaanza na Mbeya City na nimewaambia wachezaji hatupaswi kusingizia ubovu wa uwanja, tunatakiwa kushinda katika mazingira yoyote," alisema. 
 
Hajji Manara, ofisa habari wa Simba, aliiambia Nipashe jana kuwa wamejipanga kurudisha heshima Msimbazi kwa kushinda mechi kwenye viwanja ambavyo hawakuwahi kufanya hivyo kwa muda mrefu.
 
Kocha mkuu mpya wa City, Abdul Mingange alisema hana wasiwasi na mechi dhidi ya Simba kutokana na uzoefu alionao anapocheza dhidi ya timu zenye majina makubwa.
 
"Sihofii kubaki na timu (Mbeya City) kwa sababu hii ni kazi yangu, nitajitahidi kuhakikisha inashinda mechi zinazofuata na kutoka hapa ilipo," alisema Mingange.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system