Comments


MAGUFULI NITAPAMBANA NA UVUVI HARAMU



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Pwani mjini Mkuranga.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Pwani mjini Mkuranga.
Baadhi ya wanachi walio hudhuria mkutano huo.
Baadhi ya wanachi walio hudhuria mkutano huo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli amesema kwamba atahakikisha anapambana na Wavuvi haramu wa kimataifa wanaokuja katika bahari kuu ya Tanzania na kuvua samaki  kwa magendo na kuwasindika huku wakitimka nao katika  nchi za ulaya na Asia kwa ajili ya kuuza
Magufuli amesema hayo  wakati  akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Pwani mjini Mkuranga wakati akiwaomba kumpigia kura za ndiyo katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na  Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote.

Hadi leo ni siku kumi 10 pekee zimebaki kufanyika kwa uchaguzi mkuu unao subiriwa kwa hamu kubwa kufuatia idadi kubwa ya wananchi kujiandikisha kupiga kura.Amesisitiza kuwa vita hiyo ni lazima iwe kubwa na tuhakikishe tunalinda maliasili za taifa ili watanzania waweze kufaidika na rasirimali zao na kuwajengea uchumi imara wa nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system