Comments


Collabo ya Christian Bella na Ali Kiba vipi? Abdu Kiba kuichezea Simba? Hasheem Thabeet na ushindi wa AFRIMMA

Christian Bella na Ali kiba walirekodi ngoma yao katika studio za Chidaz Record lakini haikutoka mpaka sasa, leo kwenye 255 Bella amesema imechelewa kutokana na kila mmoja kuwa busy, wamekuwa na mambo mengi ikiwemo mambo ya uchaguzi lakini wamepanga Jumatatu watakwenda kushoot Video, wanatarajia kutoa Audio na Video pamoja na mashabiki wao wasione ni uongo, wawe wavumilivu.
bela
Christian Bella
Kuna tetesi kuwa Abdu Kiba ameitwa kufanya majaribio katika klabu ya Simba, kazungumza kwenye 255 na kusema ikiwa official watu watajua, ukweli amepigiwa simu lakini bado hawezi kuzungumzia kwa sasa ila mashabiki wake wasubirie..kwa sasa anafanya mazoezi na timu yake ya Muweza FC chini ya kocha wake..amesema bado anaipenda sana kazi yake ya muziki na hawezi kuiacha na kama asingekuwa mwanamuziki angekuwa mchezaji.
abd
Abdu Kiba
Mchezaji wa NBA Hasheem Thabeet alikua mmoja wa Watanzania waliohudhuria tuzo zaAFRIMMA, Dallas Marekani..anasema kama Mtanzania aliguswa kwenda kuwasapoti wenzake, amefurahi sana kuona Watanzania wameweza kuiwakilisha nchi yao vizuri, ameseama muziki wa Tanzania unazidi kukua na anaamini mwakani watapata tuzo 10.
hashe
Hasheem Thabee
t
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system