Comments


KADA MWINGINE MKONGWE WA CCM AJIENGUA




Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Juma Mwapachu.
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Juma Mwapachu.
Kada mwingine wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Juma Mwapachu ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kutokana na madai kwamba chama kimepoteza dira.
Aidha Bwa. Mwapachu aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kupitia tamko lake amesema kuanzia leo kada huyo wa CCM hatakuwa tena mwanachama wa chama hicho tawala na kuongeza kuwa bado hajaamua kujiunga na chama kingine.
‘’Kuanzia kesho( leo) mimi si mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu kupitia ofisi ya CCM ya kata yangu Mikocheni, Dar es Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na chama kingine. Mwenyezi Mungu anilinde,” inasema sehemu ya tamko hilo.
Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa miaka 48 sasa amesema kuwa katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho, chama kilidhihirisha kutokuwa chama kinachoendeshwa kwa misingi ya demokrasia kwa kumuengua waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye anapendwa na wengi ndani ya chama.
Mwapachu amesema kuwa Lowassa na wanachama wengine wa CCM waliojitoa ni sahihi hivyo naye anaungana nao.
Kwa upande mwingine Mwapachu ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho lakini pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).‘’Kujitoa kwake uanachama wa CCM hivi karibuni ni sahihi kabisa kwasababu CCM si chama tena cha watu. Kimetekwa, na mimi nakubaliana na msimamo wa Lowassa na hao waliyofuata kutoka ndani ya CCM,’’ alisema Mwapachu.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system