Comments


ICC yaitaka Afrika Kusini Kujieleza



Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya ICC Fatou Bensouda.
Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya ICC Fatou Bensouda.

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC, imeipa Afrika Kusini muda zaidi kutoa maelezo, ni kwanini ilishindwa kumkamata Rais Omar al Bashir wa Sudan, wakati alipotembelea nchi hiyo mwezi Juni mwaka huu.
Afrika Kusini ni mwanachama wa mkataba wa Roma, hivyo ina wajibu wa kuheshimu na kutekeleza maagizo ya mahakama ya ICC, lakini serikali ya nchi hiyo ilikataa kumkamata Omar al Bashir na kumruhusu kuondoka nchini humo kinyume na agizo la mahakama hiyo.

Sasa Afrika Kusini imetakiwa na ICC kujieleza kwa mahakama hiyo ifikapo tarehe 31 mwezi Desemba mwaka huuMwanzoni ICC ilikuwa imeipa Afrika Kusini hadi tarehe 5 mwezi huu kuutetea uamuzi wake, lakini serikali ilisema inahitaji muda zaidi kujibu.
Bashir anahitajika na mahakama hiyo kujibu mashitaka ya uhalifu wa kivita.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system