Licha ya kuwa headlines za soka duniani kote ilikuwa ni mchezo wa El Clasico kati yaReal Madrid dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Santiago Bernabeu, nchiniUingereza kulikuwa na mchezo mmoja uliyokuwa unavuta hisia za watu wapenzi wengi wa Ligi Kuu Uingereza.
Uingereza ulipigwa mchezo kati ya Manchester City dhidi ya klabu ya Liverpool katika uwanja wa nyumbani wa Man City Etihad, mchezo kati ya Man City dhidi ya Liverpoolulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-1 na kuifanya Man Citykushuka kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Leceister City wanaoongoza Ligi kwa sasa kwa point 28 na Man United wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 27.
Liverpool walianza kupata goli la kwanza dakika ya 8 baada ya mchezaji wa Man City Eliaquim Mangala kujifunga, goli la pili la Liverpool lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 23 wakati goli la tatu lilifungwa na Roberto Firmino dakika ya 32 kabla ya Martin Skirtel kuhitimisha kwa kufunga goli la nne dakika ya 81 huku Man Citywakiambulia goli moja la kufutia machozi lililofungwa na Sergio Aguero dakika ya 44.
0 comments:
Post a Comment