Pamoja na changamoto kadhaa, mwaka 2015 umekuwa na mafanikio kwa Barnaba ikiwa pamoja na kufanikisha kurekodi wimbo na msanii wa Uganda, Jose Chameleone.
Barnaba amesema mwaka huu amefanikiwa kujenga msingi nzuri wa muziki wake kwenda kimataifa ambao utampa mafanikio mwakani.
“Huu ni mwaka mzuri, nimefanya vizuri kwa kiasi chake, pia mafanikio yangu makubwa yapo kwenye kutengeneza connection za kwenda kimataifa zaidi,” ameiambia Bongo5.
“Nina matumaini mwaka 2016 Barnaba atakuwa Barnaba mpya kwenye tasnia yetu ya muziki na kuwapa matumaini mapya mashabiki wangu ambao walikuwa wakiumia,” ameongeza.
“Kuna video kubwa inakuja na Chameleone sitaki kusema nitafanyia wapi lakini ni kubwa. Pia kuna kolabo nyingine kubwa na msanii wa Uganda, kwahiyo nafunga mwaka kimataifa zaidi.”
0 comments:
Post a Comment