Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Algeria katika mechi ya kwanza kufuzu kombe la dunia, mwaka 2018 nchini Urusi. Katika mchezo huo ambao Stars imetawala zaidi kipindi cha kwanza, imejipatia mabao yake kupitia kwa Elius Maguli aliyefunga kwa kichwa kros ya Hajji Mwinyi dakika ya 43, huku bao la pili likifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 54. Stars ilishindwa kutumia vizuri nafasi za wazi zaidi ya tatu, kabla ya Algeria kucharuka na kutumia nafasi mbili ilizopata kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Sulman Islam dakika ya 71 na 75. Mchezo wa marudiano ni Novemba 17, mwaka huu nchini Algeria ambako Stars Italazimika kushinda au sare ya kuanzia mabao 3-3. Stars ikifanikiwa kuitoa Nigeria, itaingia katika hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment