Comments


WATU WENGI WAUAWA NCHINI PARIS.



ParisImage copyrightReuters
Image captionMashambulio kadha yametokea mjini Paris
Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.
Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.
UwanjaImage copyright
Image captionMashabiki waliingia uwanjani baada ya milipuko kutokea Stade de France
Wasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris.
Shambulio mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.
Akiongea baada ya kufika katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa "bila huruma".
Image copyrightAFP
Image captionRais wa Ufaransa Francois Hollande amehutubia taifaChanzo Cha Habari hii BBC
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system