Comments


URUSI YAONDOLEWA MASHINDANO YA RIADHAA



Image copyrightAFP
Image captionPutin alikutana na waziri wa michezo Urusi Vitaly Mutko mjini Sochi wiki hii
Shirikisho la riadha la Urusi limeondolewa kwa muda kutoka kwa mashindano ya kimataifa, ikiwemo michezo ya Olimpiki, kwa tuhuma za kuhusika katika matumizi ya dawa za kutitimua misuli.
IAAF imechukua hatua hiyo baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya shirika la kukabiliana na dawa za kutitimua misuli duniani (Wada) iliyodai Urusi imekuwa “ikisaidia katika matumizi ya dawa za kuongeza nguvu misuli”.
Wanachama wa baraza la shirikisho hilo la riadha duniani walipiga kura 22-1 kuunga mkono Urusi ipigwe marufuku.
“Huu ni ujumbe muhimu sana kwetu,” rais wa IAAF Lord Coe amesema, na kuongeza kuwa amejitolea kufanikisha mabadiliko.
“Tunahitaji kujitafakari upya, kujichunguza sisi wenyewe katika mchezo huu, na tutafanya hilo.”
Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko amesema marufuku hiyo ni ya “muda” na ni “tatizo linaloweza kutatuliwa”.
Mwakilishi wa taifa hilo katika baraza la IAAF hakuruhusiwa kushiriki kwenye kura hiyo iliyopigwa Ijumaa.
Mambo yalivyo kwa sasa, wanariadha wa Urusi hawawezi wakashiriki mashindano ya kimataifa ya riadha, ikiwemo msururu wa mashindano ya riadha duniani na michezo ya Olimpiki ya Rio itakayoanza Agosti mwaka ujao.
Rais wa Urusi Vladimir Putin tayari ameagiza uchunguzi ufanywe.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system