Comments


ANNE MAKINDA AMUA KUNGATUKA UONGOZI WA KISIASA









SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake, Anne Makinda ameamua kung’atuka uongozi wa kisiasa baada ya kutumikia nafasi hizo kwa miaka 40.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Makinda amesema ataendelea kuwa mwanasiasa na atakuwa tayari kutoa ushauri kwa watakaoendesha shughuli hizo wakipenda, ili kuendelea kujenga demokrasia.
Kwa mujibu wa Makinda, sehemu kubwa ya maisha yake, amefanya kazi za kisiasa ndani ya Bunge na Oktoba mwaka huu alitimiza miaka 40 ndani ya siasa baada ya kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo Waziri wa Shughuli za Bunge, Mwenyekiti wa Bunge na nyinginezo.

Amesema hata angekuwa mtumishi wa umma, angekuwa amestaafu hivyo ni vizuri kuachia wengine waendeshe shughuli hizo, kwani hata viongozi wengine wa kisiasa wa umri wake, wamestaafu akiwemo Rais Jakaya Kikwete ambaye ni rika lake naye amestaafu.
Aidha Akizungumzia waliojitokeza kuania nafasi ya uspika, akiwemo Spika mstaafu Samuel Sitta na aliyekuwa Naibu wake, Job Ndugai, Makinda alisema wote ni viongozi wazuri na wenye uzoefu, lakini akahadharisha kuwa pamoja na uzoefu, kuna suala la aina ya watu wanaoongozwa ambao ni lazima Spika ajaye akubali jinsi walivyo.
Amesema Spika ajaye anapaswa kukabiliana na hali halisi, atatakiwa kuwa mtulivu, kufahamu wabunge wake kwa kujifunza tabia zao mbalimbali, ili afahamu atakavyoishi nao vizuri kwa kuwavumilia na kuepuka kuwa mwepesi wa kukasirika.
Akitoa mfano, alisema katika mabunge ya kimataifa yapo hayo na hakuna kupendelewa kwa vyama, huku akiongeza kuwa alifurahia kazi na marafiki zake na atawakumbuka sana.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system