Wasanii wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ na Steve Nyerere wikiendi iliyopita inasemekana walikula chakula chenye sumu,ambapo mpaka sasa Steve Nyerere bado amelazwa hospitali.
B amezungumza na 255 kupitia XXL na kusema hivi:
‘’Siku ya Ijumaa tulikula kitimoto na vyakula tofauti tofauti sasa asubuhi yake ndio tumbo likaanza kuniuma niliendesha sana nikaenda hospitali nikapewa dawa nilivyokunywa hazikunisaidia usiku wake tumbo likaniuma sijawahi kuumwa tumbo kama nilivyoumwa siku ile hata kuongea sikuweza nikapigwa sindano mbili moja ya mshipa na nyingine ya nikapewa vidonge viwili daktari akaniambia nipumzike’’Alisema JB .
‘’Siwezi kusema kama inahusiana na ishu ya uchaguzi ninachosema ni kuwa chakula kilijuwa sio kizuri,tulikula wote kitimoto na kuanzia leo nimekoma kula kitimoto na pamoja na kulakula ovyo,nilienda hospitali kupima daktari akaniambia nimekula chakula kibovu ukweli ni kwamba niliumwa tumbo sana siku ile’’alisema JB.
0 comments:
Post a Comment