Comments


NCHI ZA AFRIKA ZIWEKEZE NGUVU YA PAMOJA KUPAMBANA NA EBOLA


Dokta Julius Julian Lutwan kutoka Uganda akitoa mada kwa wadau mbalimbali wa afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za Afrika na Ulaya zinazoshughulikia masuala ya afya katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika nakwingineko dunia. 

Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mambo ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa Professa Nigel Lightfoot akitoa mada kwa wadau mbalimbali wa afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za Afrika na Ulaya zinazoshughulikia masuala ya afya katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani.

Na Mwandishi Wetu NCHI za kiafrika zimetakiwa kuweka nguvu ya pamoja kuhakikisha zinapata njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na kuachana na utegemezi wa misaada kutoka nchi wahisani. Dokta Andrew Kitua wa taasisi ya afya ya Ngalakeri ya Morogoro aliyasema hayo jana katika warsha ya siku mbili ya kujadili njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola inayofanyika mkoani Arusha.

 Alisema kwakuwa bara la afrika ni miongoni mwa waathirika wa magonjwa hayo wadau husika katika sekta ya afya kwa pamoja na serikali za nchi husika hazina budi kuwekeza nguvu katika kutafuta suluhisho la magonjwa hayo. Alisema ingawa tayari kuna jitihada mbalimbali zinafanyika katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo lakini bado kumeonekana kuna changamoto kubwa ya kukabiliana nayo katika maeneo yanayoathirika.

 “Waafrika tunahitajika kuweka nguvu ya pamoja katika kuhakikisha tunapata njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola,” “Warsha yetu ya siku mbili inayoshirikisha wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za afya itajadili na kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kupambana na magonjwa hayo na hatimaye kupata mikakati maalumu ya kuiwekea nguvu dhidi ya mapambano hayo,” alisema Dokta Kitua. Kwa upande wake Professa Julias Lutwan kutoka Uganda alisema nchi zote kwa pamoja bila kujali kama zimewahi kuathirika au la zinahitajika kujiweka tayari kukabiliana na magonjwa hayo.

Alisema kwa afrika ukanda wa nchi za magharibi zinaonekana kupata athari hiyo kwa kiasi kikubwa unapolinganisha na ukanda wa mashiriki lakini bado kwa pamoja tunahitajika kujiweka sawa kwa tahadhari katika hilo. Kwa upande wa changamoto wanazokabiliana nazo katika tafiti wanazofanya kwa pamoja na mapambano ya jumla ya magonjwa hayo alisema mawasiliano na kada za chini katika maeneo ya vijijini ni miongoni mwa changamoto kubwa. 

Alisema kwa kuwatumia wataalamu mbalimbali wa mawasilino wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kurahisisha lugha ya mawasiliano ili jamii ya chini iweze kupata ufahamu wa jinsi ya kupambana na magonjwa husika. Warsha hii inayoshirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka barani afrika na ulaya imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system