Comments


WAJASIRIAMALI BABATI WATAKIWA KUJIUNGA NA MPANGO WA KIKOA WA NHIF


Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela amewataka wajasiriamali wa wilaya hiyo kujiunga na mpango wa bima ya afya ya Kikoa ili wapate huduma za afya kwa unafuu na ubora zaidi pindi wakiugua.
Meela aliyasema hayo mjini Babati katika kongamano la kuwakutanisha wajasiriamali wa wilaya hiyo wa vicoba, Saccos, amcos, vibindo na vikundi maalum vilivyosajiliwa ili wajiunge na mpango wa bima ya afya ya Kikoa.
Alisema kuna changamoto nyingi za afya wilayani humo ila kupitia mpango wa kikoa mwanachama wa kikundi atanufaika kwa kuchangia sh76,800 kwa mwaka na kutibiwa kwenye vituo 6 ,000 vilivyopo nchi nzima.
“Nawashukuru na kuwapongeza viongozi wa NHIF mkoani Manyara kwa kuona umuhimu wa kuwa na kongamano hili kwani linatoa fursa kwa mfuko kuwapa habari wadau wake juu ya taarifa za kujiunga na kikoa,” alisema Meela.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, meneja wa NHIF mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu alisema gharama za matibabu zipo juu sana na zinapanda kila uchao na ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuzimudu pindi anapougua.
Shekifu alisema baada ya awali kuwepo na huduma za matibabu ya bima ya afya ya NHIF, mfuko wa afya ya jamii (CHF) na tiba kwa kadi (Tika) hivyo wajasiriamali nao wachangamkie fursa hiyo kwa kujiunga na kikoa ili wapatiwe matibabu pindi wakiugua.
Kwa upande wao, baadhi ya wajasiriamali wa mjini Babati walioshirikia kongamano hilo walipongeza jitihada za NHIF kuanzisha mpango wa Kikoa ambao kwa kiasi kikubwa utawasaidia kupata huduma za afya. Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela akizungumza na wajasiriamali wa mjini Babati kwenye kongamano la kujiunga na mpango wa Bima ya Afya kwa wajasiriamali ya Kikoa iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). kushoto ni Meneja wa NHIF mkoani humo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa Ushirika wa Halmashauri ya Mji huo, Keneth Shemdoe. Wajasiriamali wa mjini Babati Mkoani Manyara, wakiwa kwenye kongamano la kujiunga na mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali ya Kikoa iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo mtu mmoja anapaswa kulipia shilingi 76,800 na kutibiwa kwa mwaka mzima kwenye zaidi ya vituo 6,00 hapa nchini.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system