Wakati wapinzani wao wa jadi FC Barcelona wakilazimishwa sare ya goli 2-2 dhidi ya Deportivo La Coruna, Real Madrid imekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Villarreal, Real Madrid walikuwa wanatajwa kuwa na nafasi ya kupunguza point na kuwasogelea wapinzani wao FC Barcelona, Real Madrid walifungwa goli la mapema katika dimba la El Madrigal.
Kosa la Luca Modric ndio lilisababisha Roberto Soldado kupewa pasi nzuri na kupachika goli hilo dakika ya 9 ya mchezo, goli ambalo limekuwa gumu kurudi na kuwafanya Real Madrid waondoke vichwa chini katika dimba la El Madrigal. Kwa matokeo hayo, Real Madrid itakuwa imezidiwa point 5 na FC Barcelona wanaoongoza msimamo wa Ligi na yenyewe kubaki nafasi ya 3 katika msimamo wa Ligi.
Video ya magoli ya Villarreal Vs Real Madrid
0 comments:
Post a Comment