Bastian Schweinsteiger amefungiwa mechi tatu na Chama cha Soka England baada ya kugombana na Winston Reid wakati Manchester United ikitoa sare na West Ham.
Uamuzi huo umefikiwa mbele ya jopo la marefa watatu ambao kila mmoja alirudia kutazama video ya tukio hilo ili kujionea vizuri kilichotokea.
Tukio hilo lilitokea kabla ya mapumziko, baada ya Schweinsteiger kumpiga usoni Reid wakati wanasubiri mpira wa kona.
Refa Mark Clattenburg alizungumza na wachezaji wote baada ya ugomvi huo, lakini hakuwachukulia hatua yoyote.
Pamoja na hayo, baada ya kubainika Clattenburg hakuona tukio hilo, FA ikamfungulia mashitaka Schweinsteiger Jumatatu.Baadaye Reid akasema nyota huyo wa Ujerumani alistahili kutolewa kwa kadi nyekundu. "Anafahamu alichokifanya – alinipiga usoni. Refa hakuona, hivyo tunasonga mbele".
Bastian Schweinsteiger amefungiwa mechi tatu kwa kumpiga usoni mchezaji wa West Ham, Winston Reid PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Refa Mark Clattenburg alizungumza na wachezaji wote baada ya ugomvi huo, lakini hakuwachukulia hatua yoyote.
Pamoja na hayo, baada ya kubainika Clattenburg hakuona tukio hilo, FA ikamfungulia mashitaka Schweinsteiger Jumatatu.Baadaye Reid akasema nyota huyo wa Ujerumani alistahili kutolewa kwa kadi nyekundu. "Anafahamu alichokifanya – alinipiga usoni. Refa hakuona, hivyo tunasonga mbele".
0 comments:
Post a Comment