Comments


Arusha Mjini, Handeni Mjini kuchagua wabunge kesho


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva.


WANANCHI katika majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini, watafanya uchaguzi wa wabunge wao kesho. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana.
Pia alisema wananchi wa Kata ya Mvomero mkoani Morogoro, nao watamchagua diwani. Wananchi wa maeneo hayo, hawakupiga kura katika uchaguzi mkuu, uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Siku hiyo, uchaguzi uliahirishwa katika majimbo saba, ikiwemo Arusha Mjini na Handeni Mjini, kata ya Mvomero na nyinginezo 34 nchini. Tangu wakati huo, uchaguzi umeshafanyika katika baadhi ya majimbo na kata.
Lubuva aliwaomba wananchi waliojiandikisha kama wapigakura katika majimbo na kata husika, kujitokeza kesho kwenye vituo walikojiandikisha ili kuweza kupiga kura na kuwachagua na viongozi wanaowataka.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system