Comments


CHICHARITO APIGA HAT-TRICK, VAN GAL APIGWA NA BUTWAA>>>>



Chicharito 2

Mshambuliaji raia wa Mexico Javier Hernandez ‘Chicharito’ jana aliifungia timu yake ya Bayern Leverkusen magoli matatu peke yake (hat-trick) katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mchezo wa ligi kuu ya Bundesliga nchiniUjerumani.

Hernandez ambaye alitajwa mchezaji bora wa mwezi uliopita katika ligi hiyo ya Ujerumani amekua katika kiwango cha juu tangu alipoachiwa na klabu yake ya zamani ya Manchester United na kujiunga na Leverkusen ya Bundesliga msimu huu.

Chicharito 1

Kocha wa Manchester United Loius Van Gaal alimkataa mchezaji huyo tangu atue klabuni hapo kwani awali pia alimpeleka kwa mkopo Real Madrid na msimu huu baada ya kurejea kikosini Van Gaal alimuachia aondoke kwamba hakua kwenye mfumo wake ambapo hadi sasa hajashinda katika takribani michezo minne mfululizo huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa butu kupita kiasi.

Bila shaka taarifa za kuchaguliwa mchezaji bora wa mwezi uliopita na sasa hat-trick ni fimbo kwa Van Gaal ambaye sasa analipwa kwa kujua kwake na kiburi chake ambapo amekua sio mvumilivu hata chembe kwa wachezaji wake huku akiwa ni kocha mwenye amri na ubabe uliosababisha hata kuondoka kwa wachezaji kama Angel di Maria.

Chicharito 3

Jana Van Gaal atakua alilala kama mgonjwa kutokana na United kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi Bournemouth huku mchezaji aliyemkataa Javier Hernandez akifunga hat-trick na timu yake ikishinda kwa mabao 5-0 wakati huo huo United wakiongeza majeruhi mara baada ya mchezaji Jesse Lingard kutolewa nje ya uwanja akiwa majeruhi.

IMG_1351-0.jpg

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system