Comments


Wadhamini wa UNITED ,ADIDASI,hawaridhishi na mwenendo wa timu hiyo.


Wadhamini wa Manchester United ambao ndiyo
wanaoitengenezea klabu hiyo jezi, Adidas
wametoa maoni yao kuhusu mwenendo wa klabu
hiyo na kusema kuwa hawafurahishwi na aina ya
uchezaji ya klabu hiyo ambayo wanaamini
haiwavutii mashabiki wa soka.
Kampuni hiyo ya kutengeneza vifaa vya michezo
ya Ujerumani ambayo imeingia mkataba na
Manchester United wa miaka 10 wenye thamani
ya Pauni Milioni 750 wameyasema hayo kupitia
Mkurugenzi Mtendaji wa Adidas, Herbert Hainer
kuwa aina ya uchezaji wa Man United sio ambao
wao wamekuwa wakiutaka.
Alisema licha ya kuwa katika kipindi kigumu
lakini wanamatumaini klabu hiyo itarudi katika
ubora wake wa awali na licha ya kuwa na kipindi
kigumu lakini bado kampuni hiyo imekuwa na
mauzo mazuri ya jezi za Man United jambo
ambalo lilikuwa hawalitegemei.
“Biashara na Manchester United inakwenda
vizuri, tunauza t-sherti zaidi ya tulivyofikiria
tunaridhishwa na hilo licha ya kuwa
hatupendezwi na mfumo ambao Man United
wanacheza sio ambao sisi tunataka kuuona,”
alisema Hainer.
Manchester United kwa sasa imekuwa katika
kipindi ambacho kimekuwa hakiwaridhishi
mashabiki wengi wa klabu hiyo kutokana na aina
ya matokeo ambayo imekuwa ikiyapata ambapo
katika michezo 15 imeyopita imefanikiwa kupata
magoli 12 pekee hali inayopelekea mashabiki
kadhaa kutaka kocha wa klabu hiyo, Louis Van
Gaal kutimuliwa kazi.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system