Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea kushika kasi wikiendi hii kwa viwanja saba siku ya jumamosi.
Coastal Union Wagosi wa kaya watakua wenyeji wa Yanga, Wekundu wa msimbazi Simba sport klabu watakua wenyeji wa Afrikani Sport mchezo utaochezwa kwenye uwanja wa taifa Dar Es Salaam.Maafande wa Jkt Ruvu watawaalika wana lizombe Majimaji ya Songea.Mtibwa Sugar watacheza na Stand United,huku Mwadui Fc ya Shinyanga watakipiga na majirani zao wa Mwanza Toto Afrikans. Kagera Sugar wao watacheza na Mbeya City.Yanga na Azam wanafukuzana kileleni wote wakiwa na alama 39, mshambuliaji wa Yanga Amis Tabwe ndie kinara wa kupachika magaoli nyavuni akiwa na mabao 13.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya jumapili kwa mchezo mmoja kuchezwa kwa Mgambo Jkt kucheza na Ndanda FC.
0 comments:
Post a Comment