Comments


UPEPO MKALI WAPELEKA KILIO MTO WA MBU WAHARIBU MAZAO//...


Mbunge wa Monduli ,Julius Kalanga akitazama migomba iliyoharibiwa na upepo mkali uliotokea jana jioni katika kata ya mto wa mbu na kuharibu migomba mingi  katika kata ya mto wa mbu.




Wananchi wa Kata ya Mto wa Mbu iliyoko wilaya ya Monduli wako hatarini kukumbwa na baa la njaa kutokana na upepo mkali uliotokea jana majira ya saa kumi na moja jioni na kuangusha migomba ya ndizi ambayo hutegemewa kama chakula kikuu na zao la biashara.

Wakulima hao walisema kuwa upepo huo mkali umeathiri mashamba makubwa ya migomba hivyo wameiomba serikali ichukue hatua za haraka kunusuru hali ngumu ya upatikanaji wa chakula itakayojitokeza siku zijazo.

Leyan Ngaboli na Moses Lengine ni wakulima wa ndizi wamesema kuwa upepo huo utasababisha kusimama kwa biashara ya ndizi kwa kiasi kikubwa kwani tayari wakulima wameanza kupata hasara kwa kulazimika kuuza ndizi kwa bei ya chini ili zisiharibikie mashambani.


Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Kusumu Hassan  alisema kuwa karibu kaya na hekari zimeathiriwa na upepo huo hivyo ameiomba serikali isaidie wakulima hao waweze kurejea katika kilimo hicho ambacho huzalisha ajira nyingi. 


Kwa upande wake Mbunge wa Monduli Julius Kalanga aliyefanya ziara ya kuwatembelea waathirika wa upepo huo amewataka wananchi kuchukua tahadhari huku akiahidi kushirikiana na serikali kutafuta chakula cha msaada kutoka serikalini ili kuwasaidia wakulima hao kwa kipindi ambacho wanaanza upya kulima mashamba yao kwani zao hilo huchukua muda mrefu.

"Nitazungumza na Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa mkoa tuangalie uwezekano wa kupata chakula cha msaada ili kunusuru kaya zilizoathirika" Alisema Kalanga


Kata ya Mto wa Mbu hutegemea kilimo cha matunda matunda kama zao la biashara na chakula ambapo matunda mengi kutoka kata hiyo hupelekwa katika masoko ya ndani nan je ya mkoa wa Arusha
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system