Nahodha wa zamani wa Manchester United Nemanja Vidic, ameweka taarifa katika mtandao wa ManUtd.com ikitangaza yeye kustaafu soka.
Vidic ambaye alihamia Inter Milan, ameamua kustaafu soka akiwa na miaka 34. Aliichezea United kwa miaka nane kuanzia Januari 2006 mpaka Mei 2014, akiisaidia mataji matano ya Ligi Kuu, matatu ya ligi, na Ligi ya Mabingwa moja na Kombe la Dunia la Klabu.
“Muda umefikwa kwa mimi kutundika daluga zangu,” alisema Vidic. “Majeraha niliyopata miaka michache iliyopita yamezidi.”
“Ningependa kuwashukuru wachezaji wote niliocheza nao, makocha wote na wafanyakazi niliofanya nao kazi, na natoa shukrani za dhati kwa mashabiki kutokana na ushirikiano wao miaka yote hii.”
Mashabiki wa United kila mmoja angependa kumshukuru Nemanja tena kwa miaka yake nane kutokana na huduma yake kwenye klabu hiyo na kumtakia kila heri katika kustaafu kwake.
0 comments:
Post a Comment