Mourinho sasa anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi mbili baada ya kutolewa kwenye eneo lake kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja
Mashetani Wekundu wafanikiwa kurejea mchezoni kufuatia kuruhusu goli la mapema lakini walishindwa kuongeza goli la pili licha ya kutengeneza nafasi nyingi, hii inamaanisha wapo pointi 11 nyuma ya kinara wa msimamo wa ligi.
Wagonga nyundo walikuwa mbele ya United ndani ya sekunde 90 tu, wakifunga goli la pili kufungwa haraka katika ziara yao Old Trafford katika historia ya Ligi Kuu Uingereza, shukrani kwa goli safi la kichwa lenye kasi ya risasi la Diafra Sakho.
Baada ya subira ya muda United waliweza kusawazisha, baada ya Paul Pogba kunyanyua mpira juu ya safu ya ulinzi ya wapinzani wao na Zlatan Ibrahimovic akauzamisha wavuni baada ya mwendo wa pasi 22.
Licha ya kuishuhudia timu yake ikitokea nyuma kusawazisha na kuambulia sare, Jose Mourinho hakuwa na furaha na maamuzi ya Jonathan Moss kumwonyesha kadi ya njano Pogba – ambayo itamwondoa kwenye mechi ya marudiano baina ya timu hizi mbili kwenye kombe la EFL Jumatano ijayo – na akabutua chupa ya maji katika eneo lake.
Kwa mara ya pili msimu huu kocha wa Manchester United Jose Mourinho aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo wa Premier League dhidi ya West Ham.
Utovu wa nidhamu kwa waamuzi baada ya Paul Pogba kujirusha, Mourinho alijikuta akishindwa kuzuia hisia zake akiwa eneo lake la kujidai na kuibutua chupa iliyokuwa mbeke yake kwa hasira.
Akipewa maelekezo na mwamuzi wan ne, Jon Moss alimwamuru Jose Mourinho kuondoka kwenye eneo la ufundi na aende jukwaani.
Rui Faria akaachwa kwenye benchi kumalizia dakika 60+ zilizosalia katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya West Ham.
West Ham hawajawahi kufunga zaidi ya goli moja katika uwanja wa Old Trafford katika majaribio 20 Ligi Kuu Uingereza, hivyo hawakuwa na ujanja zaidi ya kung’ang’ania sare, ambayo walifanikiwa kuipata licha ya presha kuongezeka dhidi yao dakika za mwisho.
0 comments:
Post a Comment