Comments


Wenger: "Ni Muhimu kumbakisha Alexis Sanchez Arsenal"

Arsene Wenger amesema Arsenal itatumia fedha kama vyombo vya habari vinavyotaka huku akikiri kuwa ni muhimu Sanchez kubaki Emirates
Bosi wa ArsenalArsene Wenger amekiri kuwa kumbakisha Alexis Sanchez Emirates kwa muda mrefu ni jambo la muhimu kwa timu yake kuwa na tumaini la mafanikio ya muda mrefu.
Sanchez, 27, ambaye amefunga magoli mengine mawili dhidi ya Bournemouth Jumapili na kutimiza idadi ya mabao 10 katika michuano yote msimu huu, amekuwa katika mazungumzo ya mkataba mpya na klabu hiyo tangu mwisho wa msimu uliopita.
Arsene Wenger hailed Alexis Sanchez for breathing life into his 'nervous' Arsenal sideAlexis Sanchez scored twice as Arsenal beat Bournemouth on Sunday afternoon

Habari za hivi punde zindai kuwa Sanchez alikuwa akifikiria mbadala mwingine kutokana na kushindwa kufikia makubaliano kuhusu mshahara wake, lakini Wenger amesisitiza kuwa hana haraka kufikia makubaliano kwani bado miaka miwili imebaki kabla ya mkataba wa nyota huyo wa kimataifa wa Chile kufika mwisho.
“Ni muhimu,” aliwaambia waandishi. “Ni muhimu kiasi gani, sijui. Hatutashughulikia hilo usiku huu. Bado tuna muda wa kutosha mbele yetu. [Vyombo vya habari] vinapenda tutumie fedha, kwa hiyo kuweni na furaha.!”

Sanchez atapewa mapumziko ya wiki mbili mwezi ujao uli kuepuka kumchosha, baada ya kutumika muda mrefu na kukosa mapumziko ya majira ya joto tangu 2013.
....................................................................................................................................................................................................................................................................
Chelsea kuanza mazungumzo ya mkataba na Victor Moses
Chelsea imeripotiwa kuwa tayari kumpatia Victor Moses mkataba mpya kubaki Stamford Bridge kama thawabu ya kiwango chake murua baada ya kuhusishwa na tetesi za Barcelona.
Nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria amekuwa moja ya masaa wa Blues tangu bosi wao Antonio Conte alipoamua kutumia mfumo wa 3-4-3, ambao amekuwa akimtumia Moses kama winga wa nyuma baada ya miaka minne nyikani.
Kwa mujibu wa Sky Sports News, Chelsea wanaandaa mazungumzo ya mkataba mpya juma lijalo kufanikisha kumpa mkataba mpya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye ametumika kwa mkopo Liverpool, Stoke City na West Ham United katika misumu mfululizo kabla ya kugundua kiwango chake chini ya Conte.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system