Comments


MGOSI<>ITAKUWA AIBU SIMBA IKIKOSA UBIGWA.......

Mgosi amesema itakuwa ni aibu kubwa kwao kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kutokana na maandalizi makubwa waliyofanya

Meneja wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amekiri kupoteza mechi mbili mfululizo kumewaweka kwenye presha kubwa ya kuhakikisha wanabeba ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Mgosi ameiambia Goal, tofauti ya pointi mbili dhidi ya watani zao wa jadi Yanga, kunawapa hofu ya kupitwa na kujikuta wanapoteza matumaini ya kuchukua taji hilo kama walivyo kusudia.

“Hatujakata tamaa bado tutaendelea kupambana kwenye mzunguko wa pili kuhakikisha hatutoki kwenye kiti cha uongozi lakini tutakuwa kwenye presha kubwa kwa sababu pointi mbili siyo nyingi endapo tutapata sare moja tayari Yanga tutakuwa tunalingana nao,” amesema Mgosi.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, amesema wanalazimika kukaa na wachezaji wao kabla ya kuanza duru la pili na kuzungumza nao kwa kirefu ili kuongeza umakini katika mechi zao kuhakikisha wanapata ushindi utakaoendelea kuwaweka kwenye nafasi hiyo ya uongozi.

Amesema kitu muhimu kwao ni kuongeza nguvu katika maandalizi yao ili waweze kumudu ushindani uliopo na kuzifunga timu mbili za Yanga na Azam ambazo ndizo zinawafukuzia kwa karibu.

“Endapo tutazifunga Yanga na Azam hapo presha yetu inaweza kupungua lakini kama tutapata sare kama ilivyokuwa mzunguko wa kwanza bado hatutakuwa katika utalivu kama ilivyokuwa kwenye mechi zetu za awali kwenye mzunguko wa kwanza,”amesema Mgosi.

Meneja huyo amesema pia wanatarajia kukifanyia marekebisho kikosi chao kwa kusajili wachezaji wawili katika nafasi ya ushambuliaji na ulinzi wa kati ili kukiimarisha kwa ajili ya kukabiliana na mapambano hayo.

Mgosi amesema wanachotaka wao ni kuhakikisha Simba inabeba ubingwa wa ligi ya Vodacom na kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ifikapo mwaka 2018 hakuna kingine.

“Simba ni timu kubwa ni aibu kwa mabadiliko tuliyofanya msimu huu alafu tukakosa ubingwa wa ligi ya Vodacom, kwasababu lengo ni ubingwa na kushiriki michuano ya kimataifa kwaiyo nilazima tupambane hadi mwisho tukiamini tunaweza kufanya kile tulicho kikusudia,”amesema Mgosi.

Simba ilianza kwa kasi ya ajabu msimu msimu huu lakini ilijikuta ikikwama kwenye mechi mbili za mwishoni mwa mzunguko wa kwanza baada ya kufungwa na African Lyon na Tanzania Prisons na kufuta rekodi yao ya kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system