Wananchi wa Kata ya Engutoto jijini Arusha wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya serikali haliinayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za kijamii.
Wakitioa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wamesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado hawajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Kamete alisema kuwa wameomba sana hati za maeneo ambayo wanaishi lakini wamekuwa awapewi na wanazungushwa zungushwa kitu ambacho kinawatia mashaka makubwa.
“Mkuu wa mkoa kinachotuuma zaidi sisi tumekaa hapa tangu kipindi cha mikonge lakini tukiomba hati hatupewi lakini akija muwekezaji anapatiwa hati kwa wakati sasa tunajiuliza inamaana sisi atuna haki ya kukaa katika viwanja hivi watuambie tu ili na sisi tujue sio wanafanya kazi ya kutuzungusha zungusha kwakweli tumekuwa tunaishi kama ndege katika maeneo yetu na atuna amani kabisa maana kama wanatunyima hati wanania gani kweli tunaomba mkuu wa mkoa utusaidie kwa hili “alisema Zaituni Marunda
Aidha wananchi hao pia wanasumbuliwa na kero za maji na umeme kwa kipindi kirefu hivyo wameiomba serikali
iwasaidie kutatua kero hiyo inayowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye alifika katika kata hiyo katika shughuli ya uzinduzi wa daraja
lililojengwa na mwekezaji Hans Paul ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero hiyo pia ameshukuru kampuni ya Hanspaul kwa kujitoa kusaidia jamii jambo ambao linapaswa kuigwa na wawekezaji wengine
lililojengwa na mwekezaji Hans Paul ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero hiyo pia ameshukuru kampuni ya Hanspaul kwa kujitoa kusaidia jamii jambo ambao linapaswa kuigwa na wawekezaji wengine
Alisema kuwa wao kama serikali wapo tayari kushirikiana na wawekezaji ambao wanalipa kodi kama ipasavyo na wale ambao wanajishuhulisha katika kusaidia jamii inayowazunguka.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amefanya mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kuzindua daraja ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 67.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizindua daraja katika Kata ya Engutoto ambalo limejengwa na wawekezaji daraja hilo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 65 za kitanzania
Mkuu wamkoa wa Arusha akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Engutoto ilipo ndani ya jiji la Arusha
Wa kwanza kulia ni muwekezaji Hans Paul katikati ni mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthuman Kiamia wakipiga magofi mara baada ya kuzindua daraja
0 comments:
Post a Comment