Comments


...............Mourinho awajibishwa na FA mara ya tatu...............

Mourinho awajibishwa na FA mara ya tatuKocha huyo wa Manchester United atawajibishwa kwa mara ya tatu ndani ya mwaka mmoja na amepewa muda wa kujibu tuhuma zinazomkabili
Jose Mourinho, meneja wa Manchester United amewajibishwa na Shirikisho la Soka Uingereza kwa mara ya tatu msimu huu baada ya kuondolewa kwenye eneo lake dhidi ya West Ham United Jumapili.
Mreno huyo aliamuriwa na mwamuzi Jonathan Moss kuondoka baada ya kupiga teke chupa ya maji kwa jazba baada ya Paul Pogba kupewa kadi ya njano dakika ya 27 United walipotoa sare ya 1-1 Old Trafford.

Bosi huyo wa zamani wa Chelsea aliwajibishwa kwa utovu wa nidhamu, na huenda akakosa haki ya kukaa eneo la kocha kwa muda mrefu kutokana na kitendo hicho.
Mourinho ameondolewa sehemu ya kocha kwa mara tatu ndani ya mwaka mmoja tu, mara ya kwanza alikuwa meneja wa Chelsea, na mara nyingine ni wiki nne zilizopita katika sare tasa dhidi ya Burnley.

Kocha huyo ana muda hadi Desembe mosi saa 12 jioni kujibu mashtaka.
....................................................................................................................................................................................................................................................................
Jordi Alba shakani kuikosa El Clasico
Barcelona imetangaza kuwa Jordi Alba amepata majeraha ya goti na kifundo cha mguu katika mechi ya La Liga dhidi ya Real Sociedad.
Alba alipata majeraha hayo katika kipindi cha kwanza cha mechi waliyotoa sare ya 1-1 katika dimba la Anoeta na hali hiyo imemwacha beki huyo wa kushoto akihaha kupona kwa ajili ya El Clasico dhidi ya Real Madrid wikiendi hii.
Maelezo ya klabu yanasomeka: “Vipimo vilivyofanyika asubuhi hii vinadhihirisha kuwa Jordi Alba amepata majeraha kwenye goti lake la kulia na kwenye kifundo cha mguu wa kushoto.
“Jinsi hali yake itakavyokuwa tutafahamu kama atakuwa sawa kwa ajili ya mechi chache zijazo.”
Hata hivyo, kiungo Arda Turan imethibitika yupo fiti baada ya kukosa mechi ya wikiendi.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system