Kuelekea mchezo wa EPL kati ya Liverpool na Machester United unaotaraji kupigwa leo usiku, kocha wa Man United, Mreno Jose Mourinho amezungumza kuhusu mchezo huo na kusema kuwa amejipanga kwenda kufanya kazi yake ambayo aliajiriwa kuifanya.
Mourinho amesema mara kadhaa amecheza katika uwanja wa Liverpool, Anfield akiwa na timu ya Chelsea hivyo hakuwa akifahamu ukubwa wa mchezo wa Man United na Liverpool na sasa anafahamu hivyo amejipanga kwa ajili ya mchezo huo.
“Sijawahi kucheza hii mechi, lakini nimecheza mara nyingi dhidi ya Liverpool, mara nyingi dhidi ya Manchester United, nafahamu ukubwa wa hizi klabu, na sasa naelewa vizuri ukubwa wa kihistoria ya hawa wapinzani wakubwa wawili. Nitakwenda kucheza mchezo wangu. Nitaenda kufanya kazi yangu na kawaida ninafurahia kazi yangu,
“Napenda hali ya mchezo, ni sifa ya hizi mechi, lakini kuwa meneja wa Manchester United inamaana zaidi, kwasababu hatuwezi kulinganisha historia kati ya timu yangu iliyopita [Chelsea] na United na Liverpool,” alisema Mourinho na kuongeza.
“Naangalia mbele kwa ajili ya hilo. Napenda kucheza Anfield. Nimeshinda mara nyingi pale pia nilipoteza. Nimeshinda mechi kubwa na nimepoteza mechi kubwa, kwahiyo siwezi kusema napenda kwenda sababu nilifanikiwa, sababu sio kweli, lakini napenda kwenda pale [Anfield],” alisema Mourinho.
0 comments:
Post a Comment