Zama za Rooney zinaonekana kufika mwisho sasa, baada ya kupata changamoto kuingia kikosi cha kwanza Man United sasa nafasi yake kwenye kikosi cha Uingereza nayo matatani
Wayne Rooney kwasasa anapitia katika kipindi kigumu kwenye maisha yake ya soka.
Imeripotiwa kuwa meneja wa mpito wa Uingereza Gareth Southgate amemtema Wayne Rooney kwenye kikosi chake cha kwanza kitakachoikabili Slovenia Hi leo.
Rooney, 30, ambaye ndiye mfungaji wa muda wote wa Uingereza, alicheza dakika zote 90 Uingereza iliposhinda 2-0 dhidi ya Malta.
Wakati wa mechi, Rooney, ambaye alishindwa kupata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza Manchester United, alizomewa na umati wa mashabiki katika uwanja wa Wembley.
Southgate alimtetea nahodha wake huyo baada ya mechi, lakini kwa mujibu wa talkSPORT, Rooney ataanzia mechi ya kesho benchi.
Ripoti zimeongeza kuwa kiungo wa Tottenham Hotspur Eric Dier atacheza nafasi yake, wakati Gary Cahill na Jordan Henderson wakiwania kitambaa cha unahodha.
Kwa sasa hapewi tena fursa ya kucheza mbele kwenye nafasi yake kama ilivyozoeleka nafasi ambayo amecheza kwa muda mrefu wa maisha yake ya soka lakini kwa sasa amerudishwa chini sehemu ambayo huenda inamsumbua.
Kiungo wa Spurs Eric Dier anaonekana kuimudu zaidi nafasi ya Rooney kitu ambacho kinasababisha presha kubwa kwa Southgate kumpiga chini nahodha wake.
0 comments:
Post a Comment