Comments


MWENYEKITI WA UWT*AFARIKI DUNIA


Umoja
 wa Wanawake Tanzania (UWT) umepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa umoja huo mkoani Dodoma, Salome Kiwaya kilichotokea jana kwa ajali ya gari.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa UWT Taifa Amina Makillagi, iliyotolewa leo, inasema Salome alifariki jana kwa ajali ya gari iliyotokea Mjini Dodoma.

Katika taarifa hiyo, Amina alisema UWT imempoteza kiongozi mahiri na makini ambaye enzi za uhai wake alikuwa mstari wa mbele kupigania Chama Cha Mapinduzi (CCM) na UWT.

Katibu Mkuu huyo alisema, familia imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mpendwa wao lakini UWT na wanachama kwa ujumla wanahuzunika kwa kumpoteza kiongozi msikivu na mwenye uelewa wa hali ya juu.

"Mwili wa marehemu utaagwa kesho Jumapili mchana mjini Dodoma na kusafirishwa nyumbani kwao mkoani Njombe kwa mazishi. UWT inatoa pole kwa ndugu, jamaa wana Dodoma, wanachama wote , CCM na wananchi wote kwa msiba huu mzito." alisema Amina

Amina aliwaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kuomboleza msiba wa mpendwa wao. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system