Comments


MATA KULAMBA MKATABA MPYA UNITED

Imeripotiwa kuwa kiungo wa Manchester United Juan Mata atapewa mkataba mpya Old Trafford baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alitarajiwa kuondoka Old Trafford majira ya joto kufuatia ujio wa Jose Mourinho ambaye alimuengua Mata Chelsea na kumuuza United mnamo 2014.
Mata amepewa nafasi ya kung'ara msimu huu, baada ya kumzidi kiwango nahodha wa Mashetani Wekundu Wayne Rooney katika nafasi yake kama mwanzilishi mkuu wa mashambulizi.
Kwa mujibu wa The Mirror, Mata, 28, ambaye mkataba wake unatarajiwa kufika mwisho msimu ujao wa majira ya joto - atasaini sasa mkataba mpya wa miaka minne na miamba hao wa Old Trafford wiki kadhaa zijazo.
Beki Timothy Fosu-Mensah pia ni miongoni mwa wachezaji wanatarajiwa kupewa mkataba mpya licha ya kukosa muda wa kutosha kwenye kikosi cha United Ligi Kuu Uingereza msimu huu.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system