Comments


PHIL NEVILLE ASEMA USAJILI WA POGBA NI SAHIHI.

Usajili ambao unataraji kukamilishwa hivi karibuni wa Paul Pogba kujiunga na timu yake ya zamani ya Manchester United umeedelea kujadiliwa na wadau mbalimbali wa siku na kila mtu akiwa na maoni yake kuhusu jambo hilo.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Phil Neville amezungumzia uhamisho huo na kusema kuwa uhamisho wa Pogba kusajiliwa na Man United kwa kitita cha Pauni Milioni 100 anaamini ni sahihi na ni aina ya mchezaji ambaye anahitajika katika kikosi cha United.

“Nafikiri ni hivyo. Nadhani wanapata mmoja wa viongo bora zaidi kwa sasa duniani, nafikiri ni mtu ambaye huwezi kumlinganisha na Xabi Alonso au Paul Scholes jinsi wanavyocheza,

“Mwonekano wake unamwonesha mtu ambaye yupo imara, na hata alipokuwa katika kituo cha kukuzia vipaji cha Manchester United, alikuwa na mwili mkubwa kuliko wengine, alikuwa anakimbia kuliko wengine, lakini pia alikuwa na nguvu, atawapa Man United kitu ambacho walikikosa kwa miaka miwili au mitatu iliyopita,” alisema Neville.

Aidha Neville alizungumzia msimu wa 2016/2017 na kusema kuwa ligi kuu ya Uingereza inazidi kuwa bora ndani na nje ya uwanja na hata kukutanisha mameneja bora duniani lakini anaamini kuwa ni timu kati ya tatu hadi tano ndiyo zitaweza kuwa katika vita ya kupigania ubingwa.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system