Baadhi ya wauzaji na wanunuzi na madini ya Tanzanite walioshiriki katika mnada,Mkurugenzi wa Kampuni ya TanzaniteOne Faisal Shahbhai,(kulia) Hussein Gonga( wa pili kulia) mchimbaji, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VGL Group ,Sunil Agrawal( wa pili kushoto), na Mmoja wa Wakurugezi wa Kampuni ya TanzaniaOne, Rizwan Ullah ( kushoto)
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera( aliyesimama)akisoma hotuba wakati wa kumtangaza mshindi wa zabuni ya kununua madini ya Tanzanite, katika mnada wa madini hayo uliofanyika mkoani Arusha, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe(wa pili kushoto), Mkurugenzi wa kitengo cha uthaminishaji Almasi na madini ya vito,Archard Kalugendo( kulia) na Kamishna Msaidizi wa Madini, Salim Salim( kushoto)
Mhandisi Juma Lunda( kulia)akitoa bahasha katika sanduku maalum la kuhifadhia maombi ya zabuni za kununua madini ya Tanzanite katika mnada.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe,( kushoto) akishuhudia uchambuaji wa barua za maombi ya zabuni ya kununua madini ya Tanzanite wakati wa mnada.
Mkurugenzi wa kitengo cha uthaminishaji Almasi na madini ya vito,Archard Kalugendo( kulia)akitangaza washindi wa zabuni za kununua madini ya Tanzanite,mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera( wa pili kulia) Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe(wa pili kushoto).
Serikali imekusanya mrabaha wa zaidi ya shilingi milioni 331 katika mnada wa madini ya Tanzanite yaliouzwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 7.56 kutoka kampuni mbili za uchimbaji madini hayo katika eneo la Mirerani mkoani Manyara.
Akitangaza washindi wa zabuni za kununua madini ya Tanzanite mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, Mkurugenzi wa kitengo uthaminishaji Almas na madini ya vito(TANSORT), Ardhard Kalugendo alisema kuwa katika mnada huo kampuni tano zilijitokeza, mbili kati ya hizo ziliuza madini yake kwa wanunuzi mbalimbali; Kampuni tatu hazikuweza kuuza kutokana na kutokubalina bei na wanunuzi.
Kalugendo alifafanua kuwa mnada huo ulifanyika kwa njia ya uwazi na kushirikisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera alisema kuwa mnada huo umeiwezesha Serikali kupata mrabaha pamoja na kuzuia utoroswaji wa madini hayo nje ya nchi uliokuwa ukiikosesha Serikali mapato yake kwa maendeleo ya taifa.
Katika hatua nyingine Bendera aliwatoa hofu wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika migodi ya Mirerani mkoani Manyara kuwa kwa Serikali imeimarisha ulinzi kwa usalama pamoja na mali zao; Pia wafanyabiara wa Tanzanite watoe ushirikiano kwa vyombo vya usalama pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha aliwasihi wanunuzi na wachimbaji wa Tanzanite kufuata sheria na taratibu za uchimbaji na ununuzi ili kuhakikisha kuwa madini hayo adhimu yanayopatikana nchini tanzania pekee duniani yanawanufaisha watanzania wote.
Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe alisema kuwa pamoja na manufaa yaliopatikana katika mnada huo, Serikali itaendelea kuboresha mnada huo kwa kuongeza muda zaidi ili kutoa fursa kwa kila mfanyabiasha wa Tanzanite kushiriki; Vilevile kuwepo na majadiliano zaidi kati ya wauzaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Profesa Mdoe aliongeza kuwa lengo la Serikali katika mnada huo ni kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite kupata matokeo chanya na yenye tija katika shughuli zao, pia Taifa linufaike kutokana na matokeo hayo kwa njia mbalimbali.
Mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Tanzanite, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzaniteone Faisal Shuhbhai aliipongeza Serikali kwa kuweka utaratibu huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini kwakuwa utawawezesha wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao kwa ufanisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Faisal alisema kuwa utaratibu wa mnada utawawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite waliokuwa wakikwepa kodi, kulipa mirabaha kwa wakati baada ya kuwepo kwa mpango huo ambao haukuwepo hapo awali; Aidha utawasaidia wafanyabiara kupata bei elekezi inayoendana na soko la dunia na hivyo kuacha kutorosha madini ya Tanzanite nje ya Tanzania kwa madai ya kutafuta masoko.
0 comments:
Post a Comment